Sunday, April 8, 2012

Watawala Wamebaka Demokrasia na Uhuru wa kuchagua


 Tarehe tano mwezi wa nne mwaka hiuu, ilikuwa ni siku ya hukumu ya kesi ambayo mwakilishi wa wananchi kwa Arusha yaani mbunge wao alikuwa ameshitakiwa nayo.

Waliomshitaki walitoa madai mengi ikiwo kuiomba mahakama kutengua ushindi wa Mbunge huyo kwa madai kuwa alipata ubunge huo pasipo halali na alitumia lugha za matusi na unyanyasaji dhidi ya wanawake wa Arusha na Tanzania.

Katika muda wote huu ambapo kesi ilikuwa ikisikilizwa zaidi ya  miezi mitatu huyo anayedaiwa kudhallilishwa hajawahi kuja mahakamani ama kulalamika au hata kuthibitisha kuwa kweli alidhalilishwa.

Pamoja na watu hao kutoweza kumleta mhusika kuthibitisha jambo hilo mahakama kuu kanda ya Arusha iliridhika na kuchukua hatua ya kumvua ubunge mbunge wa Arusha na kwamba yeye si mbunge tena!

La kushangaza zaidi hukumu hiyo tayari ilisha tolewa hata kabla ya siku ya hukumu kwani polisi walikuwa wanajua kitakachotokea na walizingira ofisi ya mbunge maasa matatu - manne kabla ya muda wa hukumu!
Sasa sisi tunajiuliza walipataje kujua kuwa hukumu itamvua Mbunge huyo madaraka?

Hiyo ni siri yao na hatutaki kujua ila tulicho kiona sisi kama wananchi wa Arusha kuwa tumibakwa kidemokrasia kwa kunyimwa haki ya kuwa na kiongozi tunayemtaka kwa sababu tu ya mafisadi wa ccm!
Watu walimchagua Lema ni zaidi 50,000 hawa wote wamekatiliwa na CCM kwa kunyimwa mbunge wao isivyo halali. japo mimi si mwanasheria lakini tumesoma machapisho mengi ambayo yanaonyesha wazi kuwa hapakuwa na kifungu cha sheria kinachotoa uhalali wa mbunge huyo kuvuliwa ubunge.

Tunachokiona hapa ni kuwa tunalazimishwa kuwa na viongozi ambao hatuwataki. Pia eleweke wazi kuwa Mbunge huyo alikuwa na mipango mingi na wanchi wake, mojawapo ni wale watoto yatima waliokuwa wanasomishwa na mfuko wa maendeleo aliouanzisha, akiwa kama mbunge.

Hawa wote wamenyimwa haki yao ya kupata Elimu na mengine mengi

Sasa najiuliza tunakwenda wapi kama taifa? Je CCM wanataka kutuaminisha kuwa haki nchi hii ipo kwa wale tu wanaotakiwa na viongozi wakuu? Je hali hii ya kupoka haki za watu ikiendelea tutarajie nini?
Je hii inatufundisha nini kama watu tunaohitaji kuendelea kuwa wamoja na wenye kuheshimiana?

Kuna maswali mengi sana katika hili ambayo watu wengi wanajiuliza, lakini mwisho wa yote itakuwaje  

Mbunge wa Ubungo John Mnyika akiwa katika hali ya butwa baada ya  hukumu ya Lema







Wananchi wa Arusha wakiwa wamikusanyika mahakamani kufuatilia hukumu ya kesi hiyo

Wananchi wa Arusha pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki wakifuatilia kesi





Mkutano wa wanaarusha na Mbunge wao wakijadili uonevu wa serikali

Watu wakihuzunikia maamuzi mabaya ya mahakama za CCM 

Umati wa huu unahuzunika na kutafakari uonevu wa serikali

Kweli wananchi wa Arusha wameonewa!