Friday, February 24, 2012

Je nyumba za ibada bado ni tumaini kwa ustawi wa watu?

Nyumba za ibada  
Ndugu zangu wapendwa karibuni tena katika mjadala wa leo mjadala wa leo unasema: Je nyumba za ibada bado ni tumaini kwa ustawi wa?

Katika siku za karibuni tumeshuhudia mambo mengi sana yakitokea katika jamii yetu. Miongoni mwa mambo hayo ni unyanyasaji wa wanajamii, unaofanywa kwa makusudi na serikali yetu.
Kwa sisi wenye kuamini katika Mungu, tuliangalia huku na huko, hatukuona mtetezi isipokuwa ni kulee kwenye nyumba za ibada!

Mawazo yetu hayo yalikuwa yamejikita katika imani kuwa huko kwaenye nyumba za ibada kutakuwa ni mahali pekee ambako dhuluma, uzushi, uongo, maonezi na fitina havipewi nafasi!

Lakini tunayoyaona sasa ni kinyume kabisa. Nyumba hizo zimeungana na wazushi ambao aibu imewakauka kabisa mithiri ya mto unaopitisha maji wakati wa masika tu. na sasa ni kiangazi hakuna hata harufu ya maji!

Wakiwa na akili zao timamu, wakiwa wanajua kabisa kuwa wanachotenda, si sahihi, wanachosema si kweli na hata wanacho amini si halisi, lakini huwa wanaujasiri wa hali ya juu sana katiaka kutimiza azima yao.

Nyumba za ibada yaani viongozi wa dini na madhehebu kwa kujua ama kwa kutojua wametumbukia kwenye mtego huohuo na sasa utawasikia wakiwatetea mafisadi kwa nguvu zote na hata kwa kula kiapo cha kufa! Hili ni jambo la kusikitisha sana.

Je tumwamini nani, au ndo yale ya wanamuziki? kwamba kila unayemwamini ni kigeugeu?

Amani Bandia Tanzania


King'amuzi Halisi

Ni wakait mwingine tunapo kutana tena, kwa nia moja tu ya kujulishana, kuburudishana na kuelimishana juu ya mambo mbalimbali yanayotuhusu. Kama mjuavyo kuwa kulikuwa na maandamano makubwa huko Songea na kwa kutotumia akili polisi waliwafyatulia watu risasi za moto, hivyo kusababisha watu wawili kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa. Hili si jambo la kujivunia hata kido!

Kwa wenye akili timamu watakubaliana na mimi kuwa hakuna amani Tanzania!

Kila kukicha vyombo vyetu vya habari hasa vinavyomlikiwa na serikali vinatuhubiria kuwa Tanzania ni nchi yenye amani.

Je hii ndio amani tunayohubiriwa kila siku?

Tafakari!

Tuesday, February 21, 2012

King'amuzi halisi vidoleni mwako!


KING’AMUZI HALISI ni blog ambayo ina lengo la kuibua mijadala inayokusudia kuwaelimisha wanajamii juu ya mambo mbalimbali ambayo yanatokea katika jamii yetu.Mambo hayo yaweza kuwa mema au mabaya, yaani chanya na hasi.
                Mara nyingi, mijadala hii italenga kupongeza, kukosoa na kuhamasisha watu waliopewa dhamana ya kusimamia usitawi wa jamii kupitia taasisi mbalimbali nchini. Hii ni pamoja na taasisi za kidini, kisiasa, serikali, mashirika yasiyo ya serikali na vyama vya kiraia. Msukumo mkubwa ukiwa ni maendeleo ya  jamii.

Maono
Maono ya mwanzilishi wa blog hii ni kuwa, katika miaka  michache ijayo tupate jamii yenye  watu wenye uelewa zaidi wa mambo muhimu yanayowagusa au yanayogusa maisha yao, kiuchumi,kitamaduni, kielimu, kisiasa na kijamii kwa ujumla wake. Hawa watu wawe na uwezo wa kuyatatua matatizo yanayowakabili badala ya kulalamika bila kuchukua hatua.

Malengo
Kuwaunganisha  wana jamii  kimitazamo ili wawe na lengo moja (common objective) ambalo ni chanya kwao katika wao kujiletea ustawi wa kimaisha! Nasema  lengo chanya kwao kwa sababu moja kwamba, kuna uwezekano kuwa kitu ambacho kwako ni chanya kwa mtu mwingine chaweza kuwa hasi.
               
Namna ya kushiiriki
Ili kufikia lengo lake kubwa kama lilivyoainishwa hapo juu, KING’AMUZI HALISI kinatoa uwanja mpana wa wanajamii kujadili mambo yanayowasibu, mafanikio yao na changamoto zinazowakabili na kutoa suluhu, hili si jambo lahisi.
                Mada au mijadala itaibuliwa hapa na wanajamii watatoa maoni yao juu ya mada husika.

Washiriki
Washiri wa mijadala hi ni watanzania kwa ujumla bila kujali jinsia, umri, cheo, dini ,uwezo kifedha, nk.

Mwisho
Nawaomba washiriki wate wa mada zitakazoibuliwa katika blog hii wawe wavumilivu wasio na jazba kwani jazba kama jazba haita tatua matatizo yetu, ila kuvumiliana na kutafuta njia mbadala ni jambo ambalo laweza kutufikisha mbali.