KING’AMUZI HALISI ni blog ambayo ina lengo la kuibua mijadala
inayokusudia kuwaelimisha wanajamii juu ya mambo mbalimbali ambayo yanatokea
katika jamii yetu.Mambo hayo yaweza kuwa mema au mabaya, yaani chanya na hasi.
Mara nyingi, mijadala hii italenga
kupongeza, kukosoa na kuhamasisha watu waliopewa dhamana ya kusimamia usitawi
wa jamii kupitia taasisi mbalimbali nchini. Hii ni pamoja na taasisi za kidini,
kisiasa, serikali, mashirika yasiyo ya serikali na vyama vya kiraia. Msukumo
mkubwa ukiwa ni maendeleo ya jamii.
Maono
Maono ya mwanzilishi wa blog hii ni kuwa, katika miaka michache ijayo tupate jamii yenye watu wenye uelewa zaidi wa mambo muhimu
yanayowagusa au yanayogusa maisha yao, kiuchumi,kitamaduni, kielimu, kisiasa na
kijamii kwa ujumla wake. Hawa watu wawe na uwezo wa kuyatatua matatizo
yanayowakabili badala ya kulalamika bila kuchukua hatua.
Malengo
Kuwaunganisha wana jamii kimitazamo ili wawe na lengo moja (common
objective) ambalo ni chanya kwao katika wao kujiletea ustawi wa kimaisha!
Nasema lengo chanya kwao kwa sababu moja
kwamba, kuna uwezekano kuwa kitu ambacho kwako ni chanya kwa mtu mwingine
chaweza kuwa hasi.
Namna ya kushiiriki
Ili kufikia lengo lake kubwa kama lilivyoainishwa hapo juu, KING’AMUZI
HALISI kinatoa uwanja mpana wa wanajamii kujadili mambo yanayowasibu, mafanikio
yao na changamoto zinazowakabili na kutoa suluhu, hili si jambo lahisi.
Mada au mijadala itaibuliwa hapa
na wanajamii watatoa maoni yao juu ya mada husika.
Washiriki
Washiri wa mijadala hi ni watanzania kwa ujumla bila kujali jinsia,
umri, cheo, dini ,uwezo kifedha, nk.
Mwisho
Nawaomba washiriki wate wa mada zitakazoibuliwa katika blog hii wawe
wavumilivu wasio na jazba kwani jazba kama jazba haita tatua matatizo yetu, ila
kuvumiliana na kutafuta njia mbadala ni jambo ambalo laweza kutufikisha mbali.
No comments:
Post a Comment