Friday, February 24, 2012

Je nyumba za ibada bado ni tumaini kwa ustawi wa watu?

Nyumba za ibada  
Ndugu zangu wapendwa karibuni tena katika mjadala wa leo mjadala wa leo unasema: Je nyumba za ibada bado ni tumaini kwa ustawi wa?

Katika siku za karibuni tumeshuhudia mambo mengi sana yakitokea katika jamii yetu. Miongoni mwa mambo hayo ni unyanyasaji wa wanajamii, unaofanywa kwa makusudi na serikali yetu.
Kwa sisi wenye kuamini katika Mungu, tuliangalia huku na huko, hatukuona mtetezi isipokuwa ni kulee kwenye nyumba za ibada!

Mawazo yetu hayo yalikuwa yamejikita katika imani kuwa huko kwaenye nyumba za ibada kutakuwa ni mahali pekee ambako dhuluma, uzushi, uongo, maonezi na fitina havipewi nafasi!

Lakini tunayoyaona sasa ni kinyume kabisa. Nyumba hizo zimeungana na wazushi ambao aibu imewakauka kabisa mithiri ya mto unaopitisha maji wakati wa masika tu. na sasa ni kiangazi hakuna hata harufu ya maji!

Wakiwa na akili zao timamu, wakiwa wanajua kabisa kuwa wanachotenda, si sahihi, wanachosema si kweli na hata wanacho amini si halisi, lakini huwa wanaujasiri wa hali ya juu sana katiaka kutimiza azima yao.

Nyumba za ibada yaani viongozi wa dini na madhehebu kwa kujua ama kwa kutojua wametumbukia kwenye mtego huohuo na sasa utawasikia wakiwatetea mafisadi kwa nguvu zote na hata kwa kula kiapo cha kufa! Hili ni jambo la kusikitisha sana.

Je tumwamini nani, au ndo yale ya wanamuziki? kwamba kila unayemwamini ni kigeugeu?

No comments:

Post a Comment